Kocha
Mkuu wa Yanga Ernie Brandts ametangaza kiama dhidi ya JKT Oljoro
Maafande wa Arusha pindi watakapokutana kesho katika Mchezo wao
utaokaofanyika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Brandts
amefunguka na kusema kuwa haoni sababu ya kutoshinda mechi ya kesho
kwani Hakuna Timu ya kuzuia Yanga kutetea Ubingwa wake kwa mara ya
pili mfululizo maneno hayo yamemtoka Kocha wa Yanga baada ya
wachezaji ambao walikuwa majeruhi kurejea katika mazoezi na kujipanga
kwa ajiri ya Mchezo wa kesho,wachezaji hao ni kama Athumn Idd, David
Luhende, na Mbuyu Twite ambao walikosa mazoezi ya awali kujiandaa na
mchezo huo wa kesho dhidi ya JKT Oljoro.
Brandts
amesema vijana wake wanaendelea kuimarika na kuyashika vizuri mafunzo
yake, kwa jinsi timu ilivyo kwa sasa anaamini vijana wake hakuna timu
ya kuizua Yanga kutetea Ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo.







0 comments:
Post a Comment