Tuesday, November 19, 2013

BAADA YA KUTIMULIWA SIMBA KIBADENI AFUNGUKA

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kikosi cha Simba ambaye jana kupitia Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba alivuliwa nafasi hiyo kwa kudaiwa kuwa Uwezo wao pamoja na Kocha Msaidizi Julio kukinoa kikosi ulikuwa Chini.

Baada ya taarifa kudhibitika kutimuliwa Jangwani Kwa kocha huyo ambaye awali alikuwa akikinoa kikosi cha Kagera Sugar alipotafutwa haya ndiyo yalikuwa maelezo yake.

Mpaka sasa (saa 6:47 mchana) bado sijapata barua ya kusimamishwa kwangu kuifundisha Simba, lakini sina pingamizi lolote na uamuzi huo. Naamini nitalipwa haki yangu kulingana na makubalino yetu yaliyomo kwenye mkataba wangu na klabu,” alisema Kibadeni.

Nitaeleza zaidi kuhusu suala hili baada ya kupata barua rasmi ya kusitishwa kwa mkataba wangu na Simba,” alifafanua zaidi Kibadeni.

0 comments:

Post a Comment