Kikosi cha Timu ya
Yanga kesho kinaingia kibaruani dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu kutoka
mkoani Pwani ambapo mchezo huo wa Mwendelezo wa Ligi Kuu
Vodacom,Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam,lakini kesho Yanga itakosa Huduma kutoka kwa wachezaji wake
Haruna Niyonzima na Nizar Khalfan.
Mpaka sasa Young
Africans inashika nafasi ya tatu ikiwa na ponti 22 pointi 1 nyuma ya
timu zinaongoza mbili za Azam FC na Mbeya City zote zikiwa na pointi
23 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Young Africans
inahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa kesho dhidi ya JKT
Ruvu ili iweze kujikita kileleni na kukalia kiti cha uongozi wa Ligi
Kuu kwa kufikisha pointi 25 ambazo zitaweza kufikiwa na timu mbili tu
za Azam FC na Mbeya City ambazo zitachezwa mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment