Mkali wa My Number One
ambaye kwa sasa amefanya Remix ya My Number na Msanii wa Nigeria
Davido amefunguka na kuwadhihilishia Watanzania kuwa
alikwenda kwenye
Msiba wa Baba Mzazi wa aliyekuwa Mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu.
Diamond ameamua
kufanya maamuzi hayo ya kuweka Picha katika Mtandao wa Instagram
kutokana na baadhi ya mashabiki ambao wanamfuatilia kudai kuwa mkali
huyo hakwenda kumpa Support Wema kutokana na Matatizo aliyoyapata ya
kumpoteza Baba yake Mzazi Mzee Issack Abraham Sepetu ambaye alipatwa
na Ugonjwa wa kupooza kabla umauti kukumkuta.
“Mwenyezi Mungu
alituagiza kuzika na ndio maana leo tuko hapa... na sio kwenda sehemu
uliyokuwa unaforce wewe ili kesho upate picha za kuzusha
instagram...! Upo...? Nakwambia, wewe ulokuwa unaandika upuuzi kwenye
comment...” Diamond akifunguka hapo
kwa mujibu ya Comment
ya Diamond ni wazi kuwa huyu mtu aliyezusha kuwa hakutimba msibani
alikuwa amempanga mkali huyo kwenda viwanja vingine na kupotezea
suala la msiba wa Baba Mkwe wake wa Zamani lakini kwa kuwa amejawa na
Busara na kuwa na watu ambao wanamshauri vizuri aliamuwa kumpiga
chini na kwenda kushiriki shughuli za Msiba.
0 comments:
Post a Comment