kwa mujibu wa Takwimu
zilizofanywa Nchini Tanzania vijana zaidi ya milioni 2 na laki Sita
wenye umri kati ya miaka 15-24 wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (Unesco), Abdoul
Coulibaly amesema hayo jana jijini Dar esa Salaam wakati wa uzinduzi
wa ripoti ya elimu ya jinsia na afya ya uzazi kwa vijana katika nchi
21 za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Alisema karibu vijana
50 katika nchi hizo huambukizwa virusi vya Ukimwi kila saa moja, huku
idadi ya wasichana wakiongoza kwa maambukizi hayo.
Coulibaly alisema
idadi hiyo ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana kwa
Tanzania, inachangiwa na kutokuwapo kwa elimu ya kutosha ya
jinsia pamoja na VVU na Ukimwi, afya ya uzazi na ukuaji wa
binadamu.
Alisema asilimia kubwa ya vijana hawana uelewa wa
masuala ya afya ya uzazi na jinsia, jambo ambalo husababisha
kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo na kusababisha
kuongezeka kwa mimba za utotoni.






0 comments:
Post a Comment