Monday, October 21, 2013

SIMBA NA YANGA ZIMEINGIZA MILLIONI 500

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Oktoba 20, 2013 kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza Sh milioni 500. Washabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi, ni tiketi 131 tu ndizo
hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C.

 Kila klabu imepata mgawo wa Sh milioni 123 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh milioni 76.3. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja Sh milioni 62.5, tiketi Sh milioni 7.3, gharama za mechi Sh milioni 37.5, Kamati ya Ligi Sh milioni 37.5, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh milioni 18.7 na DRFA Sh milioni 14.5


Source:Champion Gazeti

0 comments:

Post a Comment