Msanii wa Hip Hop
Tanzania Kala Jeremiah ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake Jaribu
kujiuliza ambayo,amepata shavu la kuwa Balozi wa Pespsi Cola
Tanzania.
Kala Jeremiah amefunguka
kuwa amesaini Mkataba na kampuni ya Pepsi hivyo atafanya kazi kama
Balozi wa Kinywaji hicho Tanzania.
“Nimesainiwa
rasmi kuwa balozi wa Pepsi Tanzania, kwa hiyo kuanzia sasa hivi
nafanya kazi zote za kibalozi ambazo balozi anatakiwa kuzifanya
katika kampuni.”
Balozi
huyo mpya wa Pepsi ametaja vigezo vilivyotumika kumpa yeye shavu
hilo, “Kwanza wanaangalia tabia ya mtu,yaani kwamba hujawi kupigana
na wala hujawahi kuwa na maskendo,lakini pia wanaangalia umati wa
watu ulionao na watu wako wanakusikiliza kiaasi gani.”
Amewashukuru
fans wake ambao ndio wamempa nafasi hiyo, kwa kuwa kigezo kimojawapo
ni kuwa na umati unaokusikiliza, “Mimi nisema nawashukuru mashabiki
wangu zaidi kwa sababu wao ndio wamenifanya leo niwe balozi wa Pepsi,
kwa hiyo shukurani zangu za dhati ziende kwa mashabiki wangu ambao
wamekuwepo kwa ajili yangu siku zote na wamenionesha mapenzi mpaka
makampuni mengine wameona kwamba nina watu wengi ambao wananielewa,
kwa hiyo ni hivyo.”
Kwa
Tanzania sasa Biashara ya Muziki imeanza kukuwa siku hadi siku kwani
hata makampuni ya Nyumbani yameanza kuwekeza katika Tasnia za
Michezo,Burudani na kubadili mwelekeo wa Maisha ya wanamichezo na
wasanii wa nyumbani.







0 comments:
Post a Comment