Wednesday, October 2, 2013

AMISI TAMBWE AMEAHIDI KUIGALAGAZA YANGA OCTOBER 20

Mshambuliaji nyota wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe amejigamba kuitandika Timu ya Yanga siku ya Jumapili ya Tarehe 20 mwezi huu watakapokutana na watani wa
jadi katika mechi ya Ligi kuu zinazoendelea kuchezwa.

Mbali na kuonesha majigambo hayo lakini Mshambuliaji huyo amedai kuwa mechi hiyo itakuwa ni moja wapo ya sehemu ya kutengeneza kumbukumbu na kutimiza Malengo yake ya kufunga mabao 20 katika Msimu wa Ligi kuu bara msimu huu.
"Sijabahatika kuwaona Yanga wakicheza, lakini nafahamu ni timu kubwa na wapinzani wakubwa wa Simba, ila hilo sijali. Siku tutakayokutana, nitakuwa na kazi moja tu ya kuwafunga kama ninavyozifunga timu nyingine,"

Alisema awapo dimbani hujipanga nafasi nzuri ili kufunga mabao, kitu ambacho kimemsaidia kutwaa tuzo kadhaa za ufungaji bora katika ligi yao ya nyumbani na ile ya Kombe la Kagame, jambo ambalo anataka kuona likitokea pia katika Ligi Kuu ya Bara.

0 comments:

Post a Comment