Msanii
maarufu wa Maigizo hapa Tanzania aliejaliwa kuwa na Vipaji vingi nje
ya Uigizaji anoufanya ambae ni mzawa wa Ubaruku Mbarali Emmanuel
Isaya Masanja Mkandamizaji leo amefunguka kuwa mpaka sasa hajaweza
kuoa sababu hajapata mtu anae mfaa.......?
Msanii
huyo amefunguka maneno hayo katik ukurasa wake wa Twitter
alipoanzisha Utaratibu kwa Fans wake kumuuliza maswali na kisha yeye
kuyajibu swali ambalo lilinivutia ni lile lililotoka kwa Msanii
anaetamba na Filamu yake ya Foolish Age Lulu Michael ambae yeye
alimuuliza swali kuwa ataoa lini?
Haikuchukua
muda Masanja alikandamiza Jibu lake kwa Mrembo huyo kuwa akitokea tu
anayefaa hata leo naona
Mbali na Hilo Msanii huyo aliulizwa swali na mtu mwingine ambaye yeye alitaka kujuwa Role Model wake ni nani katika Ulimwengu huu ambapo Mchungaji mtarajiwa alikandamiza jibu lake kuwa Role Model wake yeye ni Mama yake Mzazi, Dave Chapelle kwani anakipaji na haogopi mtu. (ana kipaji na haogopi mtu)







0 comments:
Post a Comment