Tuesday, September 17, 2013

MWALIMU WA MONTFORT AWABAKA WANAFUNZI WAWILI WA KIDATO CHA NNE

Wanafunzi wawili wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Montfort wilayani Mbarali, wanadaiwa kubakwa na mwalimu wao ambaye alikuwa anafundisha shule hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alisema tukio hilo lilitokea wiki iliyopita kwa nyakati tofauti majira ya usiku. Alisema mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifundisha katika shule hiyo masomo ya mawili inadaiwa alitenda kosa hilo kabla ya kuhamia shule moja ya sekondari wilayani Musoma, mkoani Mara.

“Tukio hilo lilitokea baada ya mwalimu huyo kumuita mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akijisomea majira saa 9:30 usiku na kisha kumfanyia unyama huo na mara baada ya kitendo hicho alimwita mwanafunzi mwingine aliyekuwa bwenini majira ya saa 4:00 usiku na kisha kumbaka naye pia” alisema.

Alisema mwalimu huyo anashikiliwa na polisi na taratibu za kumfikisha katika vyombo vya sheria ili kujibu tuhuma hizo zinaendelea.


0 comments:

Post a Comment