Friday, September 13, 2013

LICHA YA KUFUNGWA MECHI ZOTE TANZANIA YAPANDA VIWANGO FIFA

Ingawa Tanzania imefungwa mechi zote tatu za mwisho za hatua ya makundi na kutolewa katika mbio za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014, Tanzania imepanda kwa...! nafasi moja katika viwango vya ubora duniani, kwa mujibu orodha mpya ya FIFA iliyotolewa jana.

Tanzania ambayo mwezi uliopita ilikuwa katika nafasi ya 128 duniani kabla ya kuchapwa 2-0 ugenini Gambia katika mechi ya kukamilisha ratiba ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia, imepanda kwa nafasi moja hadi ya 127 duniani.

Vinara wa kundi la Tanzania katika mbio za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014, Ivory Coast, ambao wametinga kwenye timu 10 zitakazocheza mechi za 'kapu' za kuamua timu tano za kwenda Brazil, wameendelea kutisha Afrika.

0 comments:

Post a Comment