Mlimbwende
Happiness Watimanywa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende
wenzake 30 na kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013 na kupata
nafasi ya kwanza kabisa kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo.
Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na
warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu
Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao. Miongoni
mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model,
Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania
Talent.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency,
waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle'
amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari
wazoefu wa masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi
huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
Taji la Redd's
Miss Tanzania Photogenic linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano
aliyelitwaa mwaka 2012.
Mrembo huyo ambaye pia anashikilia
taji la Miss Dodoma 2013 na Miss Kanda ya Kati 2013, ana digrii ya
Biashara aliyoipata kupitia chuo cha Strathclyde University cha UK na
aliwahi kuwa wa kwanza na kuongoza nchi zipatazo 150 katika somo la
Accounts kwa shule zinazofanya mtandao wa IGCSE, Happiness alikuwa
akisoma katika shule ya Saint Constantines International School ya
Arusha. Alivumbuliwa na kipindi maarufu cha wanafunzi SKONGA
kinachooneshwa kupitia televisheni ya EATV na kuwa mfano wa kuigwa
kwa wanafunzi wengi nchini Tanzania na kwingineko.







0 comments:
Post a Comment