Monday, September 2, 2013

JINSI YA KUMGUNDUA MPENZI MPENDA PESA ZAKO

By Chris Mauki.
Nimekutana na lawama na malalamiko mengi sana kati ya wapenzi na hata maranyingine waliojikuta wameshaingia kwenye ndoa na nimeona nivema nitafute jinsi ya kuwasaidia wenye tatizo hili au kukuwezesha na wewe kumsaidia na mwingine.

Wako wapenzi wanawake au wanaume ambao tabia yao nikutafuta namna ya kuzichimba pesa za mpenzi wake kwa namna yoyote ile.
Mara nyingi wanaume wamekuwa wakiwalalamikia wanawake kuwa ndiyo wanaojifanya wanapenda kumbe wanachokitaka ni pesa au unafuu wa maisha kiuchumi kutoka kwa wapenzi wao wakiume.
Lakini sikuhizi mambo yamekuwa na uwiano sawa, wako vijana wa kiume pia ambao kazi yao ni kuwalemea wapenzi wao kila siku kwa mahitaji yasiyoisha.
Leo watasema wanashida hii, kesho shida nyingine itaibuka, na keshokutwa atakuja na jipya pia. Hali hii huyafanya mapenzi yakawa butu sana hatakama anayeelemewa hajaweza kusema kwa uwazi maumivu anayo yapata.



0 comments:

Post a Comment