Mbunge wa Nzega
(CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya wabunge,
viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu ambao ni
wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Dk.
Kigwangallah ambaye anataka kuwataja bungeni na watu wanaojihusisha
na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa majina hayo
kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi ili
kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja.
Miongoni mwa
majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na
wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam.







0 comments:
Post a Comment