Monday, September 9, 2013

HIKI NDICHO NECTA ILICHOSEMA JUU YA WANAFUNZI WATAKAO FANYA MITIHANI MWAKA HUU.


Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde amesema hakuna mtahiniwa yeyote mwenye sifa atakayenyimwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka huu.

Kauli ya Dk Msonde imekuja siku moja baada ya kuripotiwa kuwa, takriban watahiniwa 3,000 wa kujitegemea wapo hatarini kukosa mtihani huo kutokana na kutokulipa karo ya mtihani.

Dk Msonde jana alilieleza kuwa kawaida Necta baada ya kufunga usajili wa watahiniwa wa kidato cha nne, huangalia kwenye mifumo yao ili kutambua aliyekamilisha taratibu zote za usajili.

Sisi mifumo yetu haina tatizo lolote na watahiniwa wa kujitegemea hujisajili online (kwa njia ya mtandao), wapo baadhi ya watu huingia kwenye mtandao wakitaka kujisajili, wakifika kwenye eneo linalotaka walipe ada wanaacha,” alisema.

Alisema watu hao kwenye mfumo wa Necta huonekana kuwa wamejisajili, lakini hawajalipa karo ya mtihani hivyo huwasiliana nao kwa kuwaandikia barua au ujumbe mfupi wa simu ya mkononi.

 “Hizo barua ziliandikwa mapema sana baada ya kufunga usajili, kwa sasa hakuna mtu yeyote mwenye tatizo, wote wameshashughulikiwa. Ili kutatuliwa tatizo lako haikuhitaji hata kuja baraza, wewe ukipiga tu simu wataalamu wetu wanakushughulikia, sisi hapa tunafanya kazi saa 24,” alisema Dk Msonde:
source:Mwananchi Newspaper

0 comments:

Post a Comment