Monday, August 12, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMATATU 12/8/2013

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Leo Una wasiwasi mkubwa juu ya Kesi huenda ikakushika kuhusiana na pesa kazini kwako. Una mawazo mazuri sana juu ya mtoto au...
Mipango ya harusi au barua. mambo yako sasa yatafunguka na kukunyookea baada ya wiki , ile mikwamo ya hapa na pale itafunguka kwa urahisi baada ya kuja kwa mgeni.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo unataka sana mtu umpendae au kitu ukipendacho kije na unategemea barua nzuri au ujumbe.kuna kila dalili za mambo yako kufunguka hasa safari ya mbali ambayo unaitegemea. Mpenzi wako atarudi baada ya wiki mbili.
.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo Mchana ukikutana Kama Mwanamme huyo akiwa amevaa Mikufu miwili ya fedha. Hiyo ni dalili ya kutimia kwa ndoto yako ya kupata Mwanamke au Mwanamme mzuri na kutimia kwa Ndoa yako
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Ukimwaona watoto wawili wamevaa sare, basi hiyo ni dalili ya wewe kupata mtoto wa kiume kama mkeo ni mja mzito au utapata mpenzi mpya ambaye utakutana naye bila ya sokoni, Sherehe uliyoalikwa itakukutanisha na adui yako.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Wiki hii usipeleke posa wala usishiriki katika vikao vya harusi kuna matatizo yatakayokutokea iwapo hutatekeleza haya ninayokueleza. Kama umepeleka posa yako itakataliwa. Unahitajika kuwa mkweli katika mambo yako hasa ya kimapenzi..

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Hii ni wiki ya safari za ghafla na mipango ya kipesa. Elewa kuna mtu anakusengenya na hiyo ni dalili kwamba utakosa yale yote uliyoyategemea Kutana na mtu mkubwa Serikalini ambaye atakusaidia.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku mbaya kwako katika mambo ya kijamii, Utakasirishwa na kugombana na watu kwa ajili ya rafiki yako, Mkeo au mumeo au mwanao .kuwa muangalifu sana usijiingize katika magomvi utajikuta uko hospitali au Polisi.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Mpe hifadhi ya aina yoyote rafiki yako,hiyo itakufanya utatukuzwe kwa jambo na na utapata mafanikio katika malengo yako uliyoyapanga kwa wiki nzima.ukikiuka hayo tegemea kupata mikwamo ya kifedha.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Dalili ya kuwa hutafanikiwa katika mambo ya pesa utakayoyafanya leo zitajitokeza baada ya kugombana na rafiki yako .Ili kuepuka hayo jitahidi kumuomba mungu kwa sala katika kipindi cha wiki nzima

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Kumuona Panya leo ni dalili ya mkosi, ikikutokea ujue huna utakalolipata katika kipindi cha siku tatu kuanzia leo, na kama una mipango yoyote ya fedha achana nayo unaweza ukapata balaa. Jaribu kuwa muangalifu hasa na rafiki zako wa karibu.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Leo kuna kila dalili ya kukumbushwa jambo linalokukera ambalo kitu umelisahau kwa muda mrefu. Mali au kitu kilichopotea kwa siku nyingi itapatikana.Jaribu kutafuta undani kuhusu mpenzi wako anakusaliti
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku ya leo utapata habari ya moto, wizi, kulipiza kisasi, maneno machafu au ugomvi.
na hiyo itakuwa ni ishara ya kukwama katika mambo yako ya kibiashara, adui yako atakusumbua na kukuzuia kufanya mambo yako na atakutia wasiwasi mkubwa.

0 comments:

Post a Comment