Monday, August 12, 2013

KIKOSI KIPO TAYARI KUREJESHA HESHIMA ILIYOPOTEA-KIBADENI

Baada ya ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Uganda, SC Villa, katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kocha wa...!
Simba, Abdallah Kibadeni amedai kuwa kikosi chake kiko tayari kurejesha heshima iliyopotea msimu uliopita.

"Nimeridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu, yaani kilikuwa tofauti na cha juu ukilinganisha na mechi iliyopita, na hapo niliwakosa wachezaji wawili wa kigeni, ila tayari picha halisi ya kikosi cha kwanza nimeshaipata," alisema Kibadeni ambaye aliibuka kocha bora wa msimu uliopita baada ya kuiongoza Kagera Sugar kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Alisema pia ushindani wa kusaka namba umeongezeka Simba na kwa sasa hana hofu na yuko tayari kuanza kuusaka ubingwa wa ligi ambao unashikiliwa na wapinzani wao, Yanga.

0 comments:

Post a Comment