![]() |
| Ndelagakula Romedafee (23) |
“Ndipo
nikapiga kelele naumia naumia huku nikiwa nimechafuka kwa vumbi
wakati mshtakiwa alivyokuwa ananigalagaza huku akinibaka."
kutokana
na unyama huo Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemhukumu Ndelagakula
Romedafee (23) kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto wa
kike wa miaka minne baada ya kumrubuni kwa kumpatia Sh. 100.
Hukumu
hiyo ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, David Ngunyale
baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kumtia hatiani.
"Kutokana
na mshtakiwa kufanya unyama huu wa kubaka mtoto mdogo hivi, mshtakiwa
unatakiwa kuondolewa katika jamii na kupelekwa gerezani ili
ukajifunze kuwa raia mwema katika maisha yako," alisema Hakimu
huyo wakati akitupilia mbali utetezi uliotolewa na mshtakiwam huyo
ili mahakama isimpe adhabu kali.
Source:Nipashe







0 comments:
Post a Comment