Swali kubwa ambalo
limekuwa likiulizwa na watu wengi kuhusiana na ziara ya Rais wa Marekani,
Barack Obama katika bara la Afrika ukiacha Senegal na Afrika Kusini
alikotembelea, ni kwanini ameichagua Tanzania.
Swali hilo linajibiwa
na........................................................
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Balozi
wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, kwa nyakati tofauti wiki iliyopita, wakitaja
sababu zilizomfanya Rais huyo kuichagua Tanzania kuwa moja ya nchi za bara la
Afrika kuitembelea na hivyo kufuta dhana potofu iliyokuwa ikienezwa na baadhi
ya watu kwamba ziara hiyo imelenga kupora rasilimali za taifa.
Waziri Membe, alitaja
moja ya sababu ni kuwapo kwa demokrasia na utawala bora hapa nchini,Alisema
Tanzania kwa kiwango kikubwa Tanzania imekuwa inatekeleza misingi ya utawala
bora, uhuru wa kupata habari na haki za binadamu.
Alisema hata kama
kumekuwa na malalamiko juu ya suala la utekelezaji wa haki za binadamu na
utawala bora, bado Tanzania iko katika nafasi nzuri zaidi katika takwimu
kidunia ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika,Waziri Membe alisema
Tanzania pia inafanya vizuri katika kigezo cha demokrasia ikilinganishwa na
nchi nyingine Afrika.
Alisema katika
kiwango cha amani, Tanzania inashika nafasi ya 53 duniani, Kenya ikiwa nafasi
ya 135, Rwanda 136 na Burundi 144,Sababu nyingine alisema ni nafasi ya Tanzania
Ukanda wa Maziwa Makuu na kimataifa,Kwa mujibu wa Waziri Membe, Tanzania
imekuwa kinara katika utatuzi wa migogoro katika nchi jirani akitaja mfano kuwa
ni Kenya, Zimbabwe, Comoro pamoja na Madagascar.
Alisema msimamo wa
Tanzania katika masuala ya kimataifa umekuwa unaeleweka bayana,Sababu nyingine
alisema ni kuwapo kwa miradi ya Shirika la Millenium Challenge (MCC) Tanzania
inayofadhiliwa na Marekani.
Alisema Tanzania ni
nchi ya pili baada ya Morocco katika kupokea fedha za akaunti ya changamoto za
milenia kutoka Serikali ya Marekani.Alisema katika awamu ya kwanza, Tanzania
ilipokea Dola za Marekani milioni 698 ili kutekeleza miradi ya maendeleo.
Alisema Marekani
kupitia MCC inagharimia miradi mbalimbali, ikiwamo ya maji, umeme na barabara.Pia
alisema urafiki mkubwa uliopo baina ya Tanzania na Marekani na umechangia
kiongozi huyo wa taifa kubwa la Marekani kuja nchini.
Alisema Marekani na
Tanzania zimekuwa na urafiki wa karibu katika kipindi cha muongo mmoja na nusu
(miaka 15) na kwamba, ushirikiano huo umeimarika zaidi katika miaka ya hivi
karibuni hasa baada ya kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani nchini mwaka 1998.
Waziri Membe alisema
baada ya kutokea mlipuko katika ubalozi huo jijini Dar es Salaam, Tanzania
ilishirikiana kwa karibu na Marekani kuhakisha kwamba, watuhumiwa wanasakwa,
kukamatwa na kushtakiwa, wakati katika mataifa mengine haikufanyika hivyo.
Alisema kitendo hicho
cha serikali ya Tanzania, kiliongeza uaminifu kwa Serikali ya Marekani, ambayo
katika kipindi hicho ilikuwa ikiongozwa na Rais Bill Clinton.Membe alisema
ukarimu wa Watanzania umeifanya pia Tanzania kupendwa na utawala wa Rais Mstaafu
wa Marekani, George Bush, na sasa Rais Obama.
Kwa upande wake, Balozi
wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, alisema sababu za Rais Obama kuja
Tanzania ni kuwapo kwa utawala bora, demokrasia na ushirikishaji wa watu wake
wakati wa kufanya uamuzi unaogusa maisha yao ya kila siku.Alisema Tanzania ni
nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani
na utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la
Sahara.
Balozi Lenhardt
alisema sababu nyingine inayomfanya Rais Obama kuja Tanzania ni kutokana na
jitihada za Serikali ya Marekani kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na
kasi ya ukuaji wa uchumi Tanzania,alitaja sababu nyingine kuwa ni kuisaidia
Tanzania kuendeleza fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Alisema uendelezaji
huo wa fursa, una lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo
la umaskini.balozi Lenhardt alisema Marekani ni moja ya nchi zinazoongoza kwa
kutoa fedha nyingi za misaada kwa Tanzania, akitoa mfano kuwa mwaka 2012 pekee
ilitoa Dola za Marekani milioni 750.
source:Nipashe
0 comments:
Post a Comment