6:29 AM
Mbunge wa Ubungo kwa
tiketi ya Chadema Mh John Mnyika leo ameamua kuweka hadharani namba
ya simu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Andrew Chenge baada ya
Mwenyekiti huyo kusema kuwa Kodi ya kasi za Simu ni sahihi kutokana
na utafiti wao.
“Leo tarehe 25 Julai
2013 chombo kimoja cha habari kimemnukuu Mwenyekiti wa Kamati ya
Bajeti Andrew Chenge (Mb) akisema kwamba uamuzi kuhusu kodi/tozo ya
kadi/laini za simu haukuwa wa kubahatisha. Chenge amesema kwamba
kamati yake ilifanya utafiti wa kina na kisha kufikia uamuzi wa kuona
tozo hiyo ni sahihi.”
Ni muhimu akatakiwa kupitia namba yake
0754782577 atoe maelezo zaidi kuhusu usahihi wa tozo hiyo na aeleze
ni wapi wananchi na wadau mbalimbali wanaweza kupata vielelezo vya
utafiti walioufanya.
Hii ni mara ya pili
kwa Mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika kuweka namba za simu za wanasiasa
na viongozi wa Serikali ili kuweza kutolea maelezo juu ya kauli zao
kutokana na kodi ya kadi ya Simu iliyoamuliwa kulipwa na Wananchi
kama njia moja wapo ya kuongeza kipato katika bajeti ya Serikali ya
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
...
0 comments:
Post a Comment