Sakata
la Mshambuliaji Nsa Job wa Coastal Union kwenda Nchini China kwa
majaribio ya kusakata kabumbu nchini humo limechukua sura mpya baaada
ya uongozi wa Coastal Union kusema kuwa hautambui suala la safari
hiyo wala haujui juu mchezaji huyo kwenda China kwa majaribio kwa
kuwa hawana taarifa yoyote kutoka kwa mchezaji huyo.
Binslum
amesema hawezi kuzungumzia suala la mshambuliaji wa Coastal Union Nsa
Job juu ya safari yake ya china haoni kama ni habari kwani timu haina
taarifa zozote juu ya safari hiyo.
“Unajua kuna watu wanapenda tu kuonekana na kusomwa kwenye vyombo vya habari, Nsa Job hajatoa taarifa zozote juu ya kuitwa China kwa majaribio inamaana kitu kama hicho hakipo ingawa alinipigia simu kuniambia yupo China cha kuchekesha ameniambia vitu tofauti sitovizungumza hapa.”
mbali
na kueleza suala la mshambuliaji Nsa Job uongozi wa Coastal Union
umesema mpaka jumapili wachezaji wa timu hiyo kwa msimu mwingine
watakuwa wamefahamika na wale ambao hawatapata nafasi wameshawapa
taarifa kwa kuwaandikia barua.
Coastal
union inaanza mazoezi kwa ajili ya kujipanga na msimu ujao wa ligi na
kuanzia Tarehe 7 mwezi huu watapiga kambi katika Hotel ya Raskazone.
0 comments:
Post a Comment