Wednesday, June 26, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMATANO TAREHE 26/6/2013



KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Ni wakati wa kuomba msamaha kwa yale uliyoyafanya bila ya maamuzi, kivyo kuwa makini kwa sababu siku ya leo unaweza kukwama katika mambo yako utakayoyafanya.


SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Jumatano ya leo siyo nzuri jaribu sana kuwa makini katika kila jambo utakalofanya uwezekano wa kufanya makosa ni mkubwa sana, na unaweza kuponnzwa na kujikuta ukiwa matatizoni.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Matatizo yako na mikwamo inayokukumba haiwezi kumalizika bila ya kuomba msaada kwa walio karibu na wewe,, kwa hiyo tumia nafasi hii sasa ili uweze kufata mafanikio unayoyahitaji.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo ni siku nzuri sana kimapenzi kwako , utapata furaha , utaenziwa, na kupendwa na unayempenda, tumia fursa hii kuondoa matatizo ya kimapenzi ambayo unayo kati yako na huyo umpendae

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Pamoja na kupata pesa, lakini inaonyesha matumizi yako siyo mazuri naitakubidi upate ushauri ili upunguze matumizi, leo ni siku nzuri kibiashara na unaweza ukafanikiwa katika mipango yako,

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Maamuzi kwa vitendo yatakuongezea nafasi zaidi ya kukubalika na wengine, leo ni siku ambayo kila utakalofanya litakwenda vizuri lakini tahadhari sana katika kauli utakazotoa zinaweza kukuweka pabaya,

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Jumatano ya leo jipange vizuri na fanya yale tu ambayo utaelekezwa vinginevyo utapoteza kila kila kitu ambacho umetumia muda mrefu kukijenga, leo ni siku nzuri kwako kibiashara na kimapenzi,

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Juhudi zako kama ikiwa hutawashirikisha wengine hazitazaa matunda, kumbuka kwamba huwezi kufanikiwa bila ya kuwashirikisha watu wako wa karibu iwe katika suala la kimapenzi au la kibiashra.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kabla ya kufanya maamuzi yoyote tafuta ushauri, ni muhimu sana kwako vinginevyo unaweza kupata balaa, jumatano ya leo ni nzuri kuwatembelea ndugu zako ambao hamjaonana kwa siku nyingi.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Kile ambacho haukubaliani nacho unatakiwa ukiweke wazi mbele ya wengine ili uweze kusonga mbele au kupata mafanikio katika kila jambo lako unalolitaka, leo ni siku nzuri katika mambo yako

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leio ni siku nzuri ya kuwa karibu na familia yako, mkeo, watoto wako, wapenzi wako, ndugu zako na jamaa zako, kitendo cha kuwa nao kitakuletea mafanikio kinyota.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Inaonekana kwamba ndugu zako bado wataendelea kukusumbua kwa kutaka msaada aidha wa kipesa au kimawazo, jitahidi kuwatekelezea wanayotaka, kwa kufanya hivyo kutafungua bahati yako kwa siku zilizobaki za wiki hii.


Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hasan

0 comments:

Post a Comment