Wednesday, June 26, 2013

NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI TAREHE 27/6/2013


KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Mchango wako mbele ya jamii utakuongezea kipato zaidi, kumbuka kufanya kila linalowezekana ili kuwaunganisha watu. Leo ni siku ya kipato kwako, tumia nafasi hii


SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Utakayemuona na shida siku ya leo alkhamisi mpe msaada, usidharau maombi ya wengine na uwe tayari kujitoa ili mwisho wa siku upate kile ambacho umekitarajia na kile ambacho hukukitarajia.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Usipokuwa makini na kutumia akili na busara hutaweza kukwepa matatizo yanayoendelea kukusumbua kwa sasa ni vizuri sana ukabadili mwelekeo wa mipango na mipangilio yako ili uweze kupata ukitakacho.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo ni wakati wa wewe kufikia maamuzi tumia busara tumia hekima tafuta ushauri ili uwe katika hali nzuri ya kufanya mamamuzi hayo vinginevyo unaweza kukwama na kuharibikiwa.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Unapoteza nafasi ya kufanikisha mambo mengi kwa vile unaweka mkazo katika jambo moja tu ambalo jambo hilo halina faida kwako , jaribu kubadilika na uwemakini katika utekelezaji wa mipangilio yako ya kimaisha mambo yanakwenda mbele hayarudi nyuma.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Jaribu sana siku ya leo uwe mwepesi katika kutoa maamuzi, kwa sababu kuchelwewa kwako kunaweza kukuweka mbali na yale ambayo unayoyataka kwa wakati huu, leo ni siku moja ambayo bahati yako iko vizuri jaribu kufanya mambo utaona mafanikio.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Unaonekana kuwa na khofu ya muda mrefu kuhusu khatma yako, hata hivyo nafasi bado unayo, hakuna sababu ya wewe kukata tamaa, pambana na utaona mafanikio yatakuja kwa nguvu sana.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Popote ambapo utatembelea leo hii hakikisha unakuwa mbali nawa tu amboa unahisi wanajipendekeza kwako au kujifanya wazuri kwako , kwa kufanya hivyo utajiepusha na majanga au mabalaa ambayo yangeweza kukutokea , leo ni alkhamisi nzuri na ya faida kama utfanya biashara.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Utakachokifanya kwa sasa ili kubaini ukweli wa mambo yako hakitafanikiwa , nyota zinakushauri kwamba ni vyema ukaangalia mambo mengine kwa sababu mambo hayako vile unavyoyatarajia

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Furaha yako siku ya leo inaonekana itaingia dosari, kila utakachofanya kwa ajili ya mwenzako awe mkeo, mpenzi wako,mshirika wako kinaweza kugeuka kikawa kibaya , kwa ujumla leo siku nzuri kwako kuwa na tahadhari kwa kila utkalolifanya.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Siku ya leo mahusiano ya kimapenzi na mwenzako yataimarika, na hii huenda ikawa ni njia ya kuwafungulia milango ya upendo, maisha yako kwa siku ya leo yatakuwa mepesi na kuna uwezekano mkubwa wa kupata kila ulitakalo hasa pesa.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Moyo wako wa upendo utakaounyesha siku ya leo utakuongezea nafasi kubwa ya kuwa na marafiki, kumbuka kufanya yale unayoweza na usizidishe kiwango unaweza kuharibikiwa, leo ni siku ya matukio kuwa na tahadhari sana.


 Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hasan

0 comments:

Post a Comment