9:50 PM
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Siku
ya leo Zingatia kwamba, kufanikiwa kwa haja zako unazozitaka, lazima
uondoe nadhiri uliyoiweka au utimize ahadi fulani ulizoahidi zamani.
yule ambaye unamuhisi ni mbaya wako basi ni uongo. Tegemea kupata
marafiki wengi wapya leo.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku ya leo Usiogope maadui zako hata kidogo. Jaribui kupambana
nao Kuna kiongozi wa dini utakutana nae karibuni, shirikiane nae,
atakusaidia sana
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Mambo yako
yote yatakuwa baada ya Mgeni atakaporejea Adui yako lazima atapatwa
na matatizo makubwa ya Kiserikali au ugonjwa. Kuhusu safari kuna
habari nzuri za upendo utakazopata leo. Jaribu kufanya utafiti wa
mambo yako kabla hujachukua hatua.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG
22)
Pana mtu mmoja unayemfahamu ambaye yupo katika shida kwanza
umsaidie atoke au umngoje apone. utatishwa au utapigwa bila sababu na
mipango yako yote leo itakwama, kama una mgonjwa aliye hospitali
atakufa.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku ya leo
Utapendwa kwa sababu ya busara zako hata wale wanaokuchukia
watakukubali.kuna mpenzi wako wa zamani mliopoteana atarudi
jitayarishe kumpokea.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Siku
ya leo utapata habari nzuri kutoka kwa Wakili wako kwamba kuna ndugu
yako amekuachia dhamana ili upewe uyamalize matatizo yako
yanayokusumbua fuatilia hilo utaongoka.
NGE - SCORPIO (OCT 24-
NOV 22)
Mambo yako mengi unayoyataka yatatimia katika siku za
joto au katika nchi za joto joto, au saa za mchana mchana. Shirikiana
na mtu wa Jinsia tofauti na wewe kufanikisha malengo yako.
MSHALE
- SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Leo mambo yako ya kikazi yatakuwa
mabaya mipango yako ya fedha itakwama na watoto wako watakosa mambo
uliyotaka wapate.Hii ni wiki mbaya usipende kutembea kaa sana
nyumbani
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Siku ya
leo habari za Ugonjwa zitavuruga mipango yako na utavunjiwa heshima
na rafiki yako ambaye hana heshima au wewe utapata maradhi ya kuumwa
na kichwa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku ya
leo Unashauriwa kuwa, ukitaka kazi au pesa zizidi lazima uanze tena
maana yake ufanye kazi nyingine au kazi yako au biashara uliyonayo
uifanye upya, utie vitu vipya na kusafisha na kuitengeneza
tena.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo
ikiwa utapata habari za Kuhusu nyumba, au chumba basi utapata, harusi
unayotegemea pia ipo, lakini kwa sharti ubadili mwendo wako na
umuondoe yule anae kupinga kwa kufanya nae urafiki
PUNDA-
ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo Mgeni unayemtegemea haji, na mgeni
huyo kama akija hana faida utakayoipata au anajishughulisha na mambo
ya kazi zake na atakupa habari ya mbaya. Safari unayotaka kwenda ni
mbaya.
0 comments:
Post a Comment