Thursday, May 9, 2013

CMB PREZZO AKILI KUTOKA NA DIVA LOVENESS

Msanii kutoka pande za kenya CMB Prezzo AKA the president amekili kutoka kimapenzi na Mtangazaji wa Redio moja hapa Town Diva Loveness Love.
CMB amekili hayo alipopigiwa simu na Soudy Brown na kusema kuwa akimkosa mtoto huyo ataonekana mshamba na ameendelea kusisitiza kuwa anahitaji muda wa yeye kufanya mpango wa kumchukua kabsaa bishosti huyo.
Alipo ulizwa Prezzo swali kuwa je Diva ataziba pengo la marehemu Goldie moyoni mwake ? Na majibu yake yalikuwa Hiviiii
Baada ya kuulizwa swali hilo Prezzo alisema kuwa Goldie alikuwa na nafasi yake na hakuna anae weza kuziba nafasi hiyo katika maisha yake.

DIVA MWENYEWE AKANA UKWELI
Alipopigiwa simu mwanadada huyo ili kuthibitisha hilo kwa upande wake alikana kuwa hayupo in love na mwanamuziki huyo na kusema kuwa yeye na Prezzo ni marafiki tu na si wapenzi,na alibainisha kuwa yeye anae mpenzi wake ambae anampenda na hataki kumuweka wazi kwa jamii.

Baada ya watanzania kuzipata taarifa hizo halikuwa suala jema kwa upande wake Diva kwani yeye alipinga wakati Prezoo yeye ameonesha wazi kuwa kuna jambo linaendelea kati yake na Diva,hivyo inasemekana siku ya jana yote alikosa amani,ameshinda hana Raha huku akilia .



0 comments:

Post a Comment