Bondia
wa Francis Cheka amesema kuwa mchezo wa ngumi unahitaji maandalizi
zaidi na si uchawi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyomtuhumu kuwa
inawezekana anatumia uchawi katika michezo yake hiyo ya ngumi.
Cheka
amesema kuwa kama Ubondia ungekuwa unaambatana na uchawi basi kuna
mabondia kutoka Sumbawanga,Tanga basi wangekuwa wanafika mbali zaidi
katika mchezo huo lakini kwa kuwa ngumi si uchawi ndio maana
hawajaweza hata kupata ubingwa ambao yeye amepata katika mchezo huo.
“watu
wanasema kuwa kuna watu wanatumia uchawi katika kushinda,hakuna jambo
kama hilo katika mchezo wa ngumu,ngumi huitaji mazoezi ya kutosha na
kujianda vya kutosha dhidi ya mpinzani wako,ingekuwa ngumi ni uchawi
basi mabondia kutoka Tanga,Sumbawanga,Kigoma wangekuwa wanashinda
kila siku.
Bondia
francis cheka alithibitisha kuwa hana mpinzani Tanzania baada ya
kumtwanga bondia mashali katika round ya 10 na kumpelekea kupoteza
fahamu kwa muda na kushindwa kuendelea na pambano hilo.
0 comments:
Post a Comment