9:17 PM
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR
20)
Unashauriwa wiki hii kwa ajili ya kufuzu haja yako lazima
ufuatane na mtu aliezaa au ufuatane na mtoto wa kiume mdogo utaona
ajabu. Utajionea mambo ya kuchekesha na kufurahisha sana, kuwa
mtulivu zaidi hasa nyakati za jioni.
NG’OMBE – TAURUS
(APR21 – MAY 20)
Leo Watu hawa watakusaidia sana na hiyo ni
dalili ya mambo yako kukunyookea na kupata vitu ulivyokuwa
unavihitaji kwa muda mrefu. Ili kuleta baraka nenda Kanisani au
Msikitini.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Huko uendako
hakuna maeleweno ni bora ukajirudia zako nyumbani ili kuepusha shari
la bure. Katika kipindi cha siku tatu kutoka leo unaweza kupata
habari nzuri. Kila jambo lako linapokutatiza peleka shauri lako kwa
mzee wako Mwanamume au mjomba wako
KAA – CANCER (JUN 22 –
JUL 23)
Mwezi huu madeni uliyonayo yanakupa matatizo na hali yako
ya kimaisha imebadilika sana, hiyo ni mitihani na dalili za mafanikio
katika mambo yako zitaanza kuonekana baada ya siku kumi na nne,
unashauriwa kama una mipango iwe kabla ya mchana au baada ya jua
kuzama.
SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Leo una wasiwasi
mwingi, vile vile kifua kinakuuma hiyo ni dalili ya kuharibikiwa kwa
mipango yako na usipokuwa makini unaweza ukajikuta unapoteza vitu vya
thamani kubwa kizembe.kuwa muangalifu.
MASHUKE – VIRGO (AUG
24- SEPT 23)
Mchana huu kuna balaa linakusakama na Unataka sana
utoke katika Balaa kama hilo. Muone m,zee wako na muelezee matatizo
yako atakupa ushauri ambao utakusaidia sana.
MIZANI – LIBRA
(SEPT 24 – OCT 23)
Leo bahati itakujia, furaha au barua au
habari unazozitarajia utapata Mchana huu Jaribu sana kuwa makini
unaweza kupoteza fedha kwa kutapeliwa na mtu wako wa karibu.
NGE
- SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako unayoyataka yote yatakuja
kwa sharti kwamba lazima upate msaada wa mtu, unashauriwa kuwaona
wataalamu ili kukinga hali mbaya isitokee, ukidharau unaweza kufungwa
au kupoteza mtu.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Leo
utakutana na mtu na lazima umuonyeshe na kumueleza kuwa hali yako ni
mbaya na ya wasiwasi atakusaidia. Wiki hii utatukuzwa kwa jambo
utakalolifanya na utapata mafanikio katika malengo yako uliyoyapanga
hapo nyuma.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mwezi
huu utashirikishwa katika mazungumzo ya kibiashara ambayo
yatakupeleka sehemu nzuri na za kukufurahisha. Hata mkikubaliana na
huyo mshirika wako katika biashara lazima ujue atakuambia ungoje
kidogo au kukucheleweshea mahitaji yako lakini baadae utaokoka.
NDOO
–AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Katika maisha yako utasaidiwa
sana na mtu aliyezaa mtoto wa kiume au baada ya wewe kuzaa mtoto wa
kiume. Mambo yako yako karibu kufunguka hasa ukipata habari ya
kuzaliwa mtoto.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo
utapata bahati nzuri, changamkia shughuli nyingi za kifedha au
kibiashara, kwani mambo yako yatakuwa yanakwenda haraka haraka
kinyume na ulivyotegemea. Ukipata pesa zitumie katika mambo ya maana.
0 comments:
Post a Comment