9:48 PM
NG’OMBE – TAURUS (APR 21 –
MAY 20)
Leo kama una biashara unayotaka kuifanya itakuletea faida
kubwa ambayo itakusaidia katika mipango yako ya baadae. Yale makosa
yako na madhambi uliyomfanyia rafiki yako au utasamehewa Jaribu kuwa
muangalifu.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Ile mikosi
inayokuandama nyumbani na kazini itaendelea tena leo. Ili Kuondoa
hali hiyo pata msaada kutoka kwa watalaamuwakusafishie nyota yako,
vinginevyo mambo yako yatakuwa mabaya zaidi.
KAA - CANCER (JUN
22- JUL 22)
Elewa kuwa kuna mpinzani wako wa karibu asiyependa
maendeleo yako. Anajaribu kila njia kukutafutia mabalaa.Unashauriwa
ili kuepukana na hayo ni vyema ukahama sehemu uliyopo hivi sasa.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Mambo yako uliyoyapanga ili
kupata pesa wiki hii yatasimama au kuwekewa vikwazo vya hapa na pale.
Na watakaofanya hivyo ni watu wako unaowaamini. Jaribu kuachana na
mipangi hiyo mpaka baadae.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku ya leo jitahidi sana kujibidiisha na kufuatilia mipango
yako. Maombo yako yote uliyopanga yako tayari isipokuwa kuna mtu
anayashilikia. Jaribu kuzungumza nae hata kama ikiwa ni kutoa kitu
kidogo ili yawe sawa, wewe toa. Faida ni kubwa kuliko hasara
MIZANI
- LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Kuna mpenzi wako alie mbali na wewe
unamkufikiria sana. Elewa kuwa mpenzi huyo yupo njiani anakuja
kukutembelea na kukuletea msaada.Jaribu kuweka mambo yako sawa ili
akija akute kila kitu kizuri. Utapata faida kubwa kwake.
NGE
- SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Usipokuwa muangalifu katika siku mbili
hizi kuna dalili ya kumpoteza mpenzi wako wa muda mrefu, Inaonekana
pia kuna dalili ya kupoteza kitu chako cha thamani sana, chunga sana
hali ya kusahausahau.Weka vitu vyako vizuri
MSHALE -
SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo katika matembezi yako
ukikutana na mtu amebeba Samaki, hiyo ni dalili kuwa mambo yako
yatafunguka, Lakini unatakiwa kuwa makini sana na watu watakaokujia
na kutaka msaada kwako, kila samaki mmoja utakayemuona ni Bahati moja
nzuri.
.
.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo kuwa muangalifu sana unaweza kuletewa biashara ambayo
itakuletea balaa kimaisha. Biashara yoyote kwa leo haifai. Kuhusu
kazini kuna mtu anakuchimba anataka ufutwe kazi jaribu kufanya mambo
yako kwa makini hasa kazini.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR
19)
Usiwe muoga kutoa msadaa kwa matatizo yanayowapata wenzio
hasa kama mkiwa mmeongozana pamoja. Jaribu kurekebisha hiyo tabia
yako ya ubahili mara moja vingenevyo itakuleta balaa.uktakapotoa ndio
utakavyopata.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Kuna
dalili kwamba mpenzi wako atakughasi kwa maneno maneno kila wakati
kuhusiana na uhusiano wako nje ya ndoa. hata kama wewe utakanusha
lakini yeye bado atashikilia msimamo wake kwani amepewa habari za
uhakika. Jaribu kuwa mpole ili balaa liishe..
PUNDA- ARIES
(MACH 21- APR 20)
Leo Kuna dalili za kuletewa zawadi kutoka kwa
rafiki yako. Zawadi hizo zitakufariji sana. Ile migogoro yako katika
mapenzi haitakwisha hivi karibuni na kama ulikuwa unaugua au unauguza
mgonjwa basi utachelewa kupona na mgonjwa wako hatapata nafuu haraka.
Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hassan
0 comments:
Post a Comment