Mdee
alisema kutokana na athari zake kwa ardhi na binadamu, watoto ambao
wazazi wao wamekula mazao yake wanazaliwa wakiwa taahira.
Akichangia
bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mdee alisema baadhi
ya kampuni za mbegu hizo tayari zimefukuzwa nchini India na Amerika
kutokana na madhara ambayo wananchi wake waliyapata kwa sababu ya
kutumia teknolojia hiyo.
“Mosanto
(Kampuni za mbegu zenye Viwatilishi), imefukuzwa India kwa sababu
iliwafanya wakulima wadogo kuwa maskini zaidi, iliwafanya wakulima
kutegemea mbegu kutoka kwake kila mwaka, kwa sababu hizi mbegu
zikishapandwa mara moja hauwezi kurudia tena,” alisema Mdee.
Alisema
kampuni hiyo imekubali kusaidia Afrika kwa mamilioni ya fedha, huku
majaribio ya mbegu za pamba nchini tayari yakiwa yameanza.
Mbunge
huyo alisema Ufaransa imeifukuza kampuni hiyo kwa madai kuwa, watoto
wanaokula chakula kinachozalishwa na mbegu hizo wanazaliwa wakiwa
taahira.
“Yawezekana Rais akaingizwa choo cha kike na hawa mabeberu, kama huko Ulaya wenzao wamewakataa kwa nini sisi tuwakubali, wengi wenu hapa mna zaidi ya miaka 50 msituharibie kikazi hiki, baraza la mawaziri mshaurini vizuri Rais,” alisema Mdee.
“Yawezekana Rais akaingizwa choo cha kike na hawa mabeberu, kama huko Ulaya wenzao wamewakataa kwa nini sisi tuwakubali, wengi wenu hapa mna zaidi ya miaka 50 msituharibie kikazi hiki, baraza la mawaziri mshaurini vizuri Rais,” alisema Mdee.
Alisema
kampuni hiyo ambayo inaonyesha nia ya kuja kuwekeza nchini,imefukuzwa
Argentina na Peru kutokana na kubainika kuwa mbegu hizo hazimsaidii
mkulima wala udongo.
Pia,alitaka kuangalia upya suala la kutoa ardhi kwa wawekezaji nchini, kwani linaweza kufanya wananchi wengine kukosa ardhi ya kutosha.
Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (CCM) aliitaka Serikali kuhakikisha inatumia kilimo kama njia ya kupunguza tatizo kwa vijana.
Bulaya
alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kuna asilimia 30 ya vijana
wasio na ajira, 15 kwenye miji mingine na asilimia saba vijijini.
“Huku
vijijini inaonekana hivi kwa sababu vijana ndiyo hao wamekimbilia Dar
es Salaam... Serikali iangalie suala hili kwa umakini,” alisema.
Pia,
alitaka kutumia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuzalisha chakula na
kwamba, suala hilo litafanya nchi kuwa na chakula mpaka cha kuuza nje
tofauti na sasa.
“Hizi
kambi 15 za JKT zikitumika vizuri tutakuwa hatuna tatizo la chakula,
kule kuna vijana wengi wanakwenda kwa mujibu wa sheria na wengine kwa
kujitolewa, wakimaliza wanarudi mitaani, hawa watumike kuzalisha
chakula,” alisema.
Source Chadema Blogspot
0 comments:
Post a Comment