Wabunge
sita wa Chadema waliosimamishwa siku tano kuhudhuria vikao vya Bunge,
leo wanaanza kushambulia kwa mikutano yao katika Jimbo la Iringa
Mjini baada ya kumaliza Mwanza.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema
baada ya kufanya mkutano wa leo katika eneo hilo kesho watatua Mbeya
Mjini.
“Tunataka tumshtaki Spika na Naibu wake kwa wananchi kwa kitendo chao cha kutuonea sisi na kuwabeba wabunge wa CCM,”alisema Mbilinyi.
Alisema
kwa kitendo kinachofanywa na kiti cha Spika ni cha kionevu hivyo
wanakwenda kufanya mikutano hiyo ili wananchi waelewe kinachofanyika
si kizuri.
“Alhamisi
tutakuwa kwa Naibu Spika na Ijumaa tutakuwa Iramba Magharibi kwa
Mwigulu Nchemba, kazi yetu ni moja kushughulika na hawa
jamaa,”alisema
Wabunge hao wameamua kufanya hivyo kutokana na kuonyesha kukerwa na uamuzi wa Naibu Spika, Job Ndugai kuwafukuza bungeni na kuwataka wasihudhurie vikao kwa siku tano.
Wabunge hao wameamua kufanya hivyo kutokana na kuonyesha kukerwa na uamuzi wa Naibu Spika, Job Ndugai kuwafukuza bungeni na kuwataka wasihudhurie vikao kwa siku tano.
Mbali
na Mbilinyi wabunge wengine ni pamoja na Mchungaji Peter
Msigwa(Iringa Mjini), Highness Kiwia(Ilemela), Ezekiah
Wenje(Nyamagana), Godbless Lema(Arusha Mjini) na Tundu Lissu(Singida
Mashariki).
Wabunge
hao walifukuzwa bungeni kwa kufanya vurugu ya kuwazuia polisi kumtoa
nje Lissu baada ya Ndugai kuamuru hilo.““Tunataka tumshtaki Spika
na Naibu wake kwa wananchi kwa kitendo chao cha kutuonea sisi na
kuwabeba wabunge wa CCM,”alisema Mbilinyi.
SOURCE CHADEMA BLOG
SOURCE CHADEMA BLOG
0 comments:
Post a Comment