Tuesday, April 2, 2013

NAY WAMITEGO ANUSURIKA KICHAPO KISA MADEE NA AFANDE SELE


Msanii wa bongo fleva NEY WA MITEGO alietamba na kazi kibao na sasa kufanya truck ya pamoja na diamond platnum amenusurika kupigwa na mashabiki wa muziki pindi alipokuwa akifanya show katika uwanja wa K ndege.

Msanii huyo amenusurika kipigo hicho pindi alipokuwa akiimba wimbo aliofanya na Diamond unaoitwa MUZIKI GANI hasa zaidi alipofika katika ile mistari isemayo Madee na Sele bora mkaimbe TAARABU  ndipo kundi la watu liliibuka na kutaka kumpa kipigo msaanii huyo  lakini hawakuweza kutimiza lengo lao hilo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari alitiririka kuwa “ney ameafanyiwa fujo na mashabiki alipofika uwanja wa k ndege na kuanza kuchana alipofikia ile mistari inayosema madee na afande sele bora mkaimbe taarabu ndipo kundi la mashabiki wakamvamia na kutaka kumzingua ila mpaka sasa yuko fresh hajapatwa na tatizo lolote.”

0 comments:

Post a Comment