11:02 PM
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imetangaza
viwango vipya vya nauli za mabasi ya masafa marefu, daladala katika
jiji la Dar es Salaam, nauli za usafiri wa reli ya kati na
bandari.
Viwango hivyo vimetolewa kutokana na SUMATRA kufuatia
maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na makampuni
binafsi nchini kutokana ongezeko la gharama za uendeshaji.
Ahmad
Kilima ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa SUMATRA amesema viwango vipya
vimetolewa baada ya kufuata taratibu za kisheria na utendaji kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao
kuhusu ongezeko la nauli.
Amesema
SUMATRA imeongeza viwango vya juu vya nauli ya daladala kwa wastani
wa asilimia 24.46 na mabasi ya masafa marefu viwango vimeongezwa kwa
asilimia 20.3
Pia
amesema ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya
nauli na ubora wa huduma ya usafiri, mamlaka imewataka wamiliki wa
mabasi kutotumia wapiga debe katika kuuza tiketi za usafiri na kwamba
watakaokaidi hatua za kisheria zitachukuliwa.
Bwana
Kilima amesema katika kufanya mapitio ya gharama mbalimbali za
bandari na bahari kuu mamlaka imeridhia ongezeko la gharama kwa
wastani wa asilimia 34.3 hivyo TPA wametakiwa kuboresha huduma kwa
wateja kwa kuanzisha kitengo cha huduma kwa wateja .
Hata
hivyo ongezeko hilo la nauli limeenda sanjari na viwango vya nauli
kwa usafiri wa abiria wa reli ya kati ambapo mamlaka imewataka abiria
kukata tiketi na kupanda treni wakionyesha vitambulisho…
Viwango
vipya vya nauli vinatarajia kuanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili
2013 ambapo nauli ya mwanafunzi itakuwa shilingi 200 na mtu mzima
atalipa shilingi 400 kwa safari za mijini.
Source star tv
0 comments:
Post a Comment