Tuesday, April 9, 2013

AKON AWAPA BIG KWA KENYA


Msanii Kutoka Senegal alieweka makazi yake Nchini Marekani kwa sasa Akon leo amempongeza Raisi Mteule wa kenya Uhuru Kenyatta baada ya kufika katika uwanja wa mpira ulijaa maelfu ya wafuasi wa Kenyatta.

Akon amesema kuwa Hongera Uhuru Kenyatta kwa nafasi mpya ya Uraisi,ulimwengu unajivunia Kenya kwa mabadiliko ya amani.hili ni kubwa sanaa.Nipo hapa Hong Kong na hakuna jingine zaidi ya Habari ya Kenya.

Natamani ningekuwepo hapo na kushudia sherehe hizo za kuapishwa.
“Congratulations Uhuru Kenyatta on your new presidency. The world is proud of Kenya and its peaceful transition. This is big. I'm in Hong Kong and it's all over the news. I wish I could be there to Witness. AKON”.

Kenyatta mwenye umri wa miaka 51 ni mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta. Ushindi wake wa asilimia 50.07 katika uchaguzi wa tarehe 4 Machi ulihalalishwa na Mahakama ya Juu baada ya pingamizi lililowekwa na Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Raila Odinga, kutupiliwa mbali na mahakama hiyo.

Kenyatta anayekuwa rais wa nne wa taifa hilo la Afrika ya Mashariki tangu lilipopata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1963, anakuwa rais wa pili barani Afrika kuwa madarakani hali anakabiliwa na mashitaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma za kusaidia kuchochea ghasia za kikabila zilizoukumba uchaguzi wa urais wa Kenya wa mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment