WANAFUNZI wa vyuo vikuu ambao ni waumini wa dhehebu
la Katoliki mkoani Mbeya wamedai kuwa wamekua wakipambana na changamoto ya
ushawishi wa kujihusisha na ushoga vyuoni kwao.
 |
| Ask. Evaristo Chengura |
Wakisoma risala yao
mbele ya Mhashamu askofu wa katoriki jimbo Mbeya Ask. Evaristo Chengura katika
semina kwa muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu waumini wa
Katoriki Mbeya (MUCCASA), walisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na changamoto
ya ushoga vyuoni.
Akisoma risala hiyo
Mwenyekiti wa Muccasa, Alfred Nditi alisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na
changamoto ya uhamasishwaji wa masuala ya ushoga unaoshawishiwa na mataifa
makubwa ya ughaibuni.
Alisema ushawishi
huo umekuwa ukiwalenga vijana hasa walio katika vyuo mbalimbali vya elimu ya
juu hapa nchini ili wajikite katika uovu huo.
“Ushoga umekuwa
ukihamasishwa na mataifa mbalimbali hasa yale makubwa ya Ughaibuni na
ukitulenga vijana tulio kwenye vyuo vikuu hapa nchini,” Alisema Nditi.
Alisema ili
kupambana na changamoto hizo wanamatarajio ya kupinga ushoga kwa kauli moja
ili kukidhi dhana ya Mungu na uumbaji wake.
Nditi aliongeza kuwa
upingaji wa ushuga utakuwa ni wa kauli moja kwa wanaMuccasa na kuhakikisha
dhana ya Mungu ina heshimiwa na thamani ya binadamu ienziwe.
Naye Askofu Chengula
alisema kuwa ushoga umekuwa ukipingwa sana na viongozi wote wa dini lakini
umekuwa ukiendeshwa chini chini na baadhi ya watu.
“Ushoga unapigiwa
sana kelele lakini kumekuwa na watu wanaouendesha chini kwa chini na kwa siri
kubwa katika maeneo mbalimbali na hasa katika vyuo,” alisema Ask. Chengula.
Aliwaasa wanamuccasa
kwu kuwaonya wale watakao wakuta wanakijihusisha na mambo hayo machafu na
kuwashawishi kuachana na matendo hiyo.
Alisema ni vema wakawapatia
elimu juu ya kuachana na mambo hayo na kuwaeleza madhala na ubaya wa Ushoga
katika maisha yao kwani wengine wanakuwa wameathirika kisaikolojia.
Semina hiyo kwa
wananchuo ililenga kuwaelimisha wanachuo hao juu ya imani yao na jinsi ya
kusimama katika imani ambapo ilihuzuriwa na wanachuo kutoka katika vyuo
mbalimbali vya Mkoani Mbeya.
Muccasa ni
muunganiko wa wanachuo kutoka katika vyuo vikuu na taasisi za Mkoani hapa na
inajumla ya matawi 20 ya wanamuccasa.
Kwa hisani ya Furaha
Elimitaa blog
|
0 comments:
Post a Comment