Saturday, March 30, 2013

MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA MREFU DUNIANI HUYU HAPA


Wilfredy Moshi ndie alieweka historia hiyo kuwa mtanzania wa kwanza kufanikiwa kupanda Mlima Mrefu ulimwenguni Mlima EVEREST ,ilikuwa ni mwezi wa tano wa mwaka jana 2012 ndipo Wilfredy alipotimiza lengo lake la kupanda mlima mrefu zaidi ulimwwenguni na kufikia kileleni

Lakini alisema kuwa kufanikiwa kwa zoezi hilo ni kutokana na maandalizi aliyokuwa akiyafanya kalibia mwaka mzima vile vile aliweza kuweka malengo hayo kutokana na kuvutiwa kupanda mara kwa mara kwa Mlima Kilimanjaro  uliopo Tanzania ndipo alipoweka malengo ya kupanda mlima huo mrefu zaidi duniani.

Amekuwa na furaha zaidi kuiwakilisha Bendera ya nchi yakeya jamhuri wa muungano wa Tanzania

0 comments:

Post a Comment