Tuesday, May 21, 2013

RAISI BARRACK OBAMA KUTEMBELEA TANZANIA MWEZI UJAO


Raisi Barrack Obama ataitembelea Tanzania Mwezi ujao kati ya Tarehe 26-28 ataongozana na mkewe First Lady Michelle Robinson Obama pamoja na watoto wao wawili Malia na Sasha.

Katika safari yake hiyo Obama anatarajiwa kutembelea nchi tatu ambayo ni Tanzania,Senegal na South Africa japo Tanzania itakuwa ndio mwisho wa safari ya Rais huyo japo kulikuwa na tetesi kuwa angeweza kufika mpaka nchi ya Rwanda ingawa katika taarifa rasmi haijawa chaguo kwa sasa.

Mitandao ya kijamii Tanzania imekuwa ikilipoti juu ya ujio wa Raisi wa Marekani vilevile nchini South Afrika vyombo vyake vya Habarivimekuwa vikiliripoti ujio wa Obama nchini humo .

0 comments:

Post a Comment