Msanii
wa muziki wa bongo fleva Joseph Haule alimarufu kama Profesa J
ameamua kufuata nyayo za mwanamuziki mwenzake Joseph Mbilinyi kwa
kuingia rasmi katika siasa na kuchukua kadi ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA .
Kwa
mujibu wa watu wa karibu wa Jay wamesema kuwa hayo ni maandalizi ya
uchaguzi wa mwaka 2015 ingawa Jay mwenyewe amesema kuwa amechukua
kadi ya Chadema kama mwanaharakati wa siasa na kutaka kuendeleza
harakati zake hizo kupitia chama hicho.
Masaa
kadhaa kabla ya Profesa Jay kuchukua kadi ya Chadema alidai kuwa muda
mrefu watu walikuwa wakitaka kujua yeye ni chama gani kutokana na
kumuona akihusika kisaniii katika baadhi ya vyama hivyo walitaka
kujua yeye ni chama gani.
Hivyo
aliamua kuandika katika mtandao wa kijamii kuwa“Mmeniuliza
sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu litapatikana Muda sio mrefu!!
Still in Dodoma STAY TUNED!!!”
Baada
ya ku stay Tuned ndipo alipoonyesha mapenzi yake kwa chama cha
Demokrasia na Maendeleo kama ionekanavyo katika picha.








0 comments:
Post a Comment