Tuesday, May 21, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMATANO TAREHE 22/5/2013



MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Leo wakati wowote ukigongana na mtu katika matembezi yako, hiyo ni dalili kuwa kile ulichokuwa unakitafuta kwa muda mrefukitapatikana kwa urahisi, unashauriwa waone watu wako wa karibu wakusaidie. 

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Leo akikutana na Wanawake zaidi ya watatu wameshikana mikono, hiyo ni dalili kuwa ahadi uliyopewa kwa muda mrefu sasa haitatimia, unashauriwa safari yako uliyopanga kwenda iahirishe unaweza kupata hasara kupata ajali.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Leo ukikutana na mtu amebeba Gunia la Mkaa, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yatafunguka, Jaribu kuwa karibu na ndugu zako wana mpango ambao wewe huufahamu lakini utakusaidia kimaisha. Kuwa mwangalifu na kila unachotaka kukifanya.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo ukiona gari imebeba Maiti, hiyo ni dalili kuwa rafiki yako unayemtegemea kwa ushauri sio mkweli ushauri atakaokupa wiki hii usiufuate utapotea na kupata hasara au kugombana na watu wako

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Leo ukiona gari zimegongana, hiyo ni ishara ya kukutaka wewe ubadili mipango yako mingi maana njia unayotumia haitakunufaisha, Maelewano yako na bosi wako yataingiliwa na watu wabaya na unaweza ukapoteza kazi yako.Kuwa muangalifu.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo katika harakati zako ukikutana na mwanamke mwenye sura mbaya, hiyo ni dalili kwamba mambo yako yataimarika na kukunyookea, masuala ya mahaba yatakuwa na misukosuko ya hapa na pale.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Leo ukimuona mnyama anakula nyama, hiyo ni dalili kuwa mipango yako itakunyookea. Kuna uwezekano wa kupata safari ya ghafla itakayokuletea neema kubwa. Mambo ya mapenzi yatakuburudisha


MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo katika matembezi yako ukikuta wanyama wanapigana, hiyo ni dalili kwamba utatokewa na mambo ya ajabu ajabu ambayo yatakukosesha raha kabisa, kuwa makini na hali hiyo na usiwe na munkar nayo

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Leo ikikukutokea ukakutana na mpenzi wako wa zamani hiyo ni dalili kuwa matatizo yako ya mpenzi wako mpya au katika ndoa yako yataendelea kuna uwezekano wa kutokea kutengana au Talaka, Jaribu kuwa muangalifu.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo ukikutana na Bubu, basi ujue hiyo ni dalili ya kwamba kutakuwa na ucheleweshaji wa mambo yako ya kifamilia. Lakini pamoja na hayokuna nafasi kubwa ya mafanikio na mwisho wake utakuwa wa furaha.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo, ukikukutana na mtu anayetukana matusi, hiyo ni dalili kwamba mambo yako ya kufanya mapenzi na mtu uliyemtaka kwa siku nyingi itaibuka upya, lakini utakumbana na misukosuko ya kifamilia. Ndoa yako iko salama.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Wiki hii ili kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uendelee unaonywa uachane kabisa na tabia ya kumshutumu mwenzio na uwe unapenda kusikiliza mawazo ya mpenzi wako. Kuna matatizo ya mawasiliano kati yenu. Njia ya kufanya kuokoa urafiki au ndoa yenu ni kutumia busara.

0 comments:

Post a Comment