Baada
ya kutamba na ngoma kali kama Iveta,Sitaki
tena kuumizwa na Mganga,msanii kutoka pande za mwanza Rock city Sajna
anakuja na Ningekuwa Single.
Kwa
muda fulani Sajna amekuwa kimya katika Tasnia ya Bongo fleva na
kuwaacha wakali wengine kutoka pande za Mwanza kuwakilisha vilivyo
akiwamo C-Sir Madini kwa wasanii wanaoimba huku wakali wengine
kutoka pande hizo katika Hip Hop waliendelea kuwakilisha Jiji la
Mwanza akiwamo Young Killer mzee wa Dear Gambe.
Sajna
ameamua kudondosha wimbo huo mwanzoni wa mwezi wa Sita
aliowashirikisha wakali wa R&B Ben Paul pamoja na C-Sir Madini,
kwa mujibu wa Sajna amekili kutowaangusha Fans wake kabsaa katika
ngoma hiyo iliyounganisha vichwa vitatu vya R$B.
“Zimebaki
siku chache naachia wimbo wangu mpya itakuwa mwezi wa 6 ni wimbo wa
mapenzi ambao nimewashirikisha BEN POL na jembe langu C-SIR
MADINI...Sisemi mengi mtakuja kujaji wenyewe ila nachoweza kusema
sijawaangusha,Niamini mimi sijawaangusha!”







0 comments:
Post a Comment