Monday, May 20, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMANNE TAREHE 21/5/2013


MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21) 
Mpenzi wako atarejea salama, na utashinda mitihani na adui yako atajutaHii ni wiki yako nzuri ya kurekebisha makosa yote ambayo umeyafanya katika kipindi cha nyuma.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku ya leo Lazima utapata kitu unachokitaka au pesa unazohitaji au mtu unayemtarajia. Mtoto au kitu kilichopotea kitarejea lakini tahadhari utapatwa na balaa la kupigwa bila ya kutegemea na bila kosa lolote na hata kama lipo kosa basi kosa hilo hukulifanya wewe.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Siku ya leo lazima utapata kitu unachokitaka au pesa unazohitaji au mtu unayemtarajia. Mtoto au kitu kilichopotea kitarejea mambo yako mengi yatasimama, yale tu utakayoyafanya wewe mwenyewe ndiyo yatakayofanikiwa, lakini yale yote utakayoyaagiza yafanywe na watu wengine yatalala.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku ya leo Safari unayofikiria ni nzuri, na biashara yako itafanikiwa maendeleo yako yatakuwa ni madogo na yatakuwa yanaenda polepole sana. Biashara yako pia itapanuka kwa kusuasua.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Siku ya leo Unashauriwa kuwa kufanikiwa kwa mambo yako kunahitaji wewe uanze kujishughulisha na mambo hayo mara moja wala usisite site.Jambo baya kwako ni kuwa kama kuna mgonjwa hapo nyumbani kwako, lakini kama kuna mjamzito basi atazaliwa mtoto wa kike

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Siku ya Leo Mambo yote unayotaka utayapata kwa sharti uache kuwa na wasiwasi na hofu au kupapatika, mambo yako mengi yatakwenda kwa kusuasua, Unashauriwa kuwa makini na kila unachotaka kukifanya, usimamizi wa karibu unahitajika kwa kila jambo unalotaka kulifanya.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo,itakubidi utoe rai nzuri na uache woga na usivunjike moyo kwani patatokea upinzani na undani, kuna habari za uongo utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana na biashara zako. Jaribu kufanya uchunguzi kabla hujachukua hatua.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo Haja yako itatimia. Kuna mtu mkubwa wa hapo ndiye atakaye kuonea huruma kwa njia usiyoitegemea. mgonjwa wako aliye hospitali atazidiwa au utaletewa habari ya mbaya za kifo cha mgonjwa.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku ya leo unawaza juu ya nafsi yako,unataka kujua maisha na hali yako itakuwaje. Pana kazi au jambo ambalo unashaka nalo kama litatimia au vipi? Elewa kwamba utapata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku hii ya leo kuna mgeni na kitu kilichopotea ambacho unataka sana kujua habari zake. Leo utapata fedha au utapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa madhambi uliyomfanyia rafiki yako.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Siku ya leo una hamu ya kukutana na mpenzi wako na kujua juu ya safari au biashara na kazi. mambo yako yataenda kombo, Unashauriwa kuwa mtulivu na hali hiyo kwa kuwa ni hali ya muda mfupi tu.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mambo yote unayoyataka yatatimia kati ya leo Jumanne au Jumamosi ijayo usiku. Pengine katika mwezi wa Mei Tegemea kujionea mambo mengi ambayo ulikuwa umefichwa kwa muda mrefu na watu wako wa karibu. Ili kuleta baraka leo nenda kawatembelee wazee wako. 

0 comments:

Post a Comment