![]() |
| NGASA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO |
Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa
amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla
ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka
3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye
mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema
anashukuru kwa Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji
anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa
akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali
ya juu.
Kwa
kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea
katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia
kwa kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha
Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu
ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua
wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na
kunishangilia pia.
Nimeamua
kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee
wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza
kwa moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho
ndo kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngsa
anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya
kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.








0 comments:
Post a Comment