Friday, May 17, 2013

NANI KAMWAGA POMBE YANGU-SIMBA AU YANGA


Yakiwa yamebakia masaa kadhaa kwa watani wa Jadi Simba na Yanga kukutana katika Uwanja wa Taifa na kuoneshana makli yao uwanjani homa ya soka imeeanza kutawala kwa mashabiki hata viongozi wa Club hizo mbili kutokana na ukweli kwamba kila Club imekamia kushinda mechi ya kesho ili kuonesha ukali na kuthibitisha umahiri wake nakuoneshana mabavu ya kijadi jadi yale.

Kwa namna moja au nyingine mechi kati ya watani hawa si nyepesi hata kidogo kwani kila Club imekamia kufanya vizuri hivyo utakuwa ni mchezo wa kukamiana katika kutafututa ushindi kwa hili kila mmoja anajiuliza nani atamwanga pombe ya mwenzake ni Simba au Yanga.

Mchezo kati ya watani wa jadi hawa utachezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro akisaidiwa na washika vibendera Samuel Mpenzu kutoka Arusha, Jesse Erasmo kutoka Morogoro huku mwamuzi wa akiba akiwa Hashim Abdallah kutoka Dar es salaam.

Kocha Mkuu wa Yanga Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo fiti, kiakili, kifikra, kiafya na morali ya wachezaji ni ya hali ya juu hivyo wana kila sababu ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo kwakua Yanga kwa sasa ina kikosi bora kuliko timu zote katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Tabiri ushindi wa kesho kati ya watani wa jadi hawa.


0 comments:

Post a Comment