Thursday, January 29, 2015

DADA WA DIAMOND ACHOCHEA BIFU YA ALI KIBA NA DIAMOND PLATNUM

Na Gerald Kitalima 
Mwanamuziki ambae ni dada wa mwanamuziki Diamond Platnumz ambae ni Queen Darleen amezidi kuchochea bifu ya muziki uliyopo
kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba.


wanamuziki hao ambao kwa sasa wamekuwa na ushindani mkubwa kimuziki.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na show kubwa ya muziki ambayo ilifanyika katika viwanja vya Ledears Club ambapo katika show hiyo iliwakutanisha Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba ambao kila mmoja alipata mapokezi tofauti kutoka kwa mashabiki wao,katika show hiyo kuna baadhi ya mashabiki ambao walikuwa na furaha kushuhudia show ya wakali hao wawili wakati show inaendelea msanii Diamond Platnum aliweza kuwarushia noti za buku mbilimbli mashabiki wake.Kufuatia kitendo hicho ndipo msanaii Queen Darleen amefunguka na kusema kuwa dawa ya machupa steji ni pesa."Machupa kiboko yake pesaa,tunasaka hela na wewe saka "
Mashabiki wa Queen Darleen wameonyeshwa kutofurahishwa na kauli ambayo imetolewa na dada wa nyota wa muziki Diamond Platnum na wao wanaamini kuwa msanii huyo anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa Diamond pamoja na Ali Kiba,hawa ni baadhi ya mashabiki ambao wametoa mtazamo wao juu ya kauli ya Queen Darleen.
Fadhiliromanusy4real Fikiria mara mbili kabla ya kuandika,chuki hazitakusaidia mtu kukuona unampenda sana,Diamond atakukubali tu kwa kuwa inasemekana wewe ni ndugu yake sio lazima kumtusi Ali Kiba sio fresh kabisa kumbuka uhusiano wako na Ali kabla Diamond hajatoka,kweli tenda wema nenda zako walimwengu hawana fadhila @queendarleen4real kama vip futa hiyo 4real andika Diamond ili ueleweke.
Popo_wa_insta @teamkibaforlife Wewe...kidalali cha kiba tulia usijifanye unajua kuongea wakati nyie mnajua kuloga tuu..na kuruka ukuta....diamond unamtajataja ili iweje sasa watu kama nyinyi..hii account ipo kwa ajiri yetu..acha watu watumie pesa nyie tumieni ilizi..acha kumtaja dangote usitake..kuendeleza beef liwe kubwa...ayo tuu kama unataka kuendelea endelea..
Metalstanzania Although nimemjua Darleen kwa sababu ya Alikiba.Just saying.Anaweza kuonyesha love kwa kaka yake bila kusambaza chuki kati yao.
Sayiness85 Sikutegemea kama unaweza andika huo upuuzi kuanzia leo sio shabiki wako tena
I_am_ichu_ Hapo ajatajwa mtu bana na hapo ndio tunapokosea wabongo ....na kumdhalilisha huyo kiba sababu amesema machupa kwa hiyo mnavyo comment hiyvo inaonesha kama kiba kausika sio poa kabisa.
WamkondeleilaKm kweli Kiba aliwatuma watu warushe makopo kweli dongo linamhusu na alistahili ila kama hakuwatuma mnalalamika nini? Kabla hata kumsema Darleen mumseme huyo Kiba kwanini mwenzie arushiwe makopo?
shebbymmokoHahahaha watu wamepanic wakat post inasema #Machupa kiboko yake #Pesa yan kamaanisha wale waliorusha machupa walikua na shida na hela kumbe sasa sijui hayo mambo ya MrukaUkuta Ally Kiba yamekujaje tenah! Wabongo kwa kumaliza movie clip.
Ramso67064Daaah Mwanangu umeteleza fikiri Mara mbili kabla ya kuandika si leo tuu,,, maisha yako yote,,, bado sijakushusha wewe ni mwenye IQ kubwa
Bin_salim20Ila kumbuka kuwa haki hainunuliwi jiongezee hata ukiwa na msichana akikupenda kwa pesa ujue kuna mwenzako bila pesa anapenda upendo wa dhati kinachowaumiza hamjakijua ila jiulizeni why kiba tunampenda wa Tanzania kuliko msanii yoyote tena kwa mioyo yetu bila kutushawishi kwa chochote mkipata jibu mujipange sana.
Msanii Queen Darleen kupitia ukurusa wa facebook wa EATV mwaka jana wakati akichat Live kupitia kipengele cha Kikaangoni Live alishasema kuwa katika wanamuziki wa Tanzania wa kiume anamkubali sana Ali Kiba 4Real,na alidai kuwa ni rafiki yake wa karibu.





0 comments:

Post a Comment