Waziri
mkuu Mizengo amemuumbua Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe na
kudai kuwa ameudanganya Umma kwa kutoa taarifa sisizo sahihi juu
ya
Mshahara wake kama waziri mkuu,Mizengo Pinda ameweka wazi mshahara
wake na kusema kuwa analipwa mshahara wa milioni 6, mshahara ambao ni
pamoja na posho ya mke wake.
Mwezi
uliopita Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe akiwa anahutubia
wananchi wa Mji wa Mpanda katika viwanja vya maridadi alifunguka na
kusema kuwa waziri mkuu anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa
mwezi na kila kitu anapata bure.
Lakini
Mizengo Pinda amekanusha na kusema kuwa haelewi hiyo taarifa Zitto
aliyoitoa kwa Wananchi imetoka wapi pia aliongeza kuwa mshahara wake
hauna tofauti kubwa sana na mshahara wa Rais, kwani kuwa
hautofautiani sana.
Kutokana
na hali hiyo Mizengo Pinda amedia kuwa yeye amekuwa ni mkopaji mzuri
sana katika Mabenki mbalimbali ili aweze kukidhi haja ya mahitaji
yake.
0 comments:
Post a Comment