Thursday, December 5, 2013

SIMBA NA YANGA KUKIPIGA JUMAMOSI 21

Mchezo wa ngao ya Hisani kati ya Mabingwa watetezi Yanga na watani wao wa Jadi Simba utachezwa siku ya Jumamosi ya Tarehe 21 katika Uwanja wa Taifa
badala ya Tarehe 14 ambayo ilikuwa imetangazwa awali.

Mchezo huo ambao utaambatana na kumpata NaniMtaniJembe kati ya Simba na Yanga ambapo Mshindi atajizolea kitita cha Pesa alizovuna kutoka kwa mashabiki wake.

Katika Mashindano hayo mpaka sasa Yanga inaongoza kwa kupata 77,921,000 huku watani wao wakiwa nyuma kwa kupata 22,079,00 hivyo mashabiki Unaombwa kuendelea kupiga kura ili kuiwezesha Klabu yako kujivunia Kitita cha Pesa.



0 comments:

Post a Comment