Kiungo wa Yanga
Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa yupo Nchini Kenya na
Kikosi cha Timu yake ya Taifa ya Rwanda AMAVUBI inayoshiriki
mashindano ya kombe la Chalenji ameliliwa na kuonesha kuhitajika Mno
katika Kikosi cha Yanga ili kukamilisha baadhi ya Program ambazo Timu
hiyo imezianza kujiandaa na Mashindano ya Afrika Mwakani.
Kufuatia Mazngira hayo
Kocha wa Yanga amemtaka kiungo huyo kurejea kurejea haraka Tanzania
ili kujiunga ndani ya kikosi chao kinachojiandaa kwa mchezo wa Ngao
ya Hisani dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.
"Kwa
kuwa Rwanda tayari imeshatolewa Chalenji, sioni haja Niyonzima
kukawia kujiunga na timu yangu (Yanga). Tunakabiliwa na mashindano
magumu ya Afrika mwakani, tunatakiwa kujiandaa vizuri na kwa wakati,"
alisema Brandts.
0 comments:
Post a Comment