Kocha mkuu wa Yanga
Ernie Brandts, ameongeza mkataba wa kuendelea Kukinoa Yanga kwa Mwaka
Mmoja,Kocha huyo
ambaye jana alisaini Mkataba huo akiwa kwenye Gari
yake wakati Timu hiyo ikiendelea na Mazoezi katika Uwanja wa Bora
Kijitonyama jijini Dar es Salaam .
Baada ya mazoezi ya timu
hiyo kumalizika kwenye uwanja huo majira ya saa tano asubuhi huku
kukinyesha mvua, Brandts aliingia kwenye gari lake akifuatwa na
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ambaye naye aliingia kwenye gari hilo
aina ya Toyota Land Cruiser na kukabidhi mkataba kwa kocha
huyo.
Baada ya mchakato kukamilika Kocha huyo alikubali
kusaini Mkataba wa kuendelea kukinoa Kikosi cha Yanga..
"Ndiyo,
nimesaini mkataba mpya na Yanga mbele ya Meneja wa Timu (Saleh). Kama
kawaida yangu, sihitaji mkataba mrefu zaidi, hivyo nimeingia nao
mkataba wa mwaka mmoja tu,"
0 comments:
Post a Comment