Wednesday, December 4, 2013

FID Q AMEWACHANA WADAU,SOMA HAPA MANENO MACHACHE KUTOKA KWAKE

Msanii Fid Q ambaye siku mbili zilizopita alihojiwa na Radio ya Uingereza BBC Kiswahili na kuzungumzia masuala ya Rushwa huku akiwa ameonesha ni kwa
jinsi gani Rushwa ni adui wa Haki .
 
Leo kupitia Mtandao wake wa kijamii msanii Fid Q amewachana baadhi ya wadau ambao walialikwa na Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania PCCB na walipofika huko waliulizwa Fid Q yuko wapi na Majibu yao yalikuwa kuwa Yupo Ulaya.


Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na siri ya Mtungi amewauliza watu hao kama wao ndio walimlipia ViSA ya kwenda huko Ulaya,hii inaonesha wazi kabsa kuwa Wadau hao waliamua kumficha FIQ Q Juu ya Mwaliko huo na kuamua kuuwa soo kwa namna hiyo.

0 comments:

Post a Comment