Wednesday, December 4, 2013

NEY WA MITEGO AMEMTAJA SIWEMA KUWA NDIYE MPENZI WAKE.

Msanii wa Hip Hop ambaye makazi yake ni Manzese anafahamika kwa jina la True Boy leo amefunguka juu ya Mahusiano yako Alipoulizwa swali na Moja ya
Shabiki wake kupitia Ukurasa wa Facebook wa EATV alipokuwa akichat Live na Fans wake.
 
Fans huyo aliuliza Kuwa kwa sasa unatoka na Demu gani na ndipo hapo mkali huyo wa Michano alipoweka wazi kuwa anampenzi na anaitwa SIWEMA .

Moja ya swali ambalo msanii huyu aliulizwa sana na watu wengi ni kuhusu kujiamini kwake na kuwachana baadhi ya Wasanii kupitia muziki wake.

Na majibu ya Swali hili kutoka kwa Ney yalikuwa kama ifuatavyo Sijiamini bali huwa nafanya Jambo ambalo naona linawezekana kwangu kulifanya.



Katika kuzungumzia Bifu Ney wa Mitego alikanusha kutokuwa na Bifu na msanii Peter Msechu na kudai kuwa Peter Msechu ni rafiki yake wa karibu sana.

0 comments:

Post a Comment