Timu
ya African Lyon ambayo inacheza Ligio Daraja la Kwanza kupitia
Viongozi wake umeendelea kuwavuruga baadhi ya Wachezaji wa Yanga
ambao wanataka
kusajiliwa na Timu hiyo kwa njia ya Mkopo kutoka Kwa
Mabingwa watetezi Yanga.
Siku
mbili zilizopita moja ya kiongozi wa Juu ya African Lyon alikuwa na
Mazungumzo na Kocha wa Mabingwa Watetezi Yanga baada ya Mazungumzo
hayo Kiongozi huyo alitoa taarifa kuwa alifika Uwanjani hapo
ilikuzungumza na Kocha huyo juu ya kuwapata wachezaji watano ambao
Timu yake inawahitaji.
"Sisi
(African Lyon) tuna uhusiano mzuri na Yanga, nimekuja hapa uwanjani
kuzungumza na benchi la ufundi la Yanga kuhusu wachezaji wao watano
ambao tunataka kuwasajili kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Brandts amesema hana tatizo na suala hilo na yuko tayari kuwaachia
kwa sababu hawahitaji sana kwenye kikosi chake kwa sasa,"
Kutokana
na Taarifa hizi kuwafikia Wachezaji wa Yanga kuna baadhi ya Wachezaji
wameonesha wasiwasi na kuwa na hofu huenda wao ndio wakauzwa kwa
mkopo kwenda African Lyon kutokana na kutopata nafasi uwanjani
kutokana na uwezo wao kuwa chini kidogo dhidi ya wale wanaopata
nafasi kucheza Uwanjani.
0 comments:
Post a Comment